Na Baraka Lusajo. Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewataka wananachi mkoani humo  pamoja na wakandarasi  wanaoendelea  kutekeleza  ujenzi wa miradi mbalimbali kwenye  wilaya  tofauti  za mkoa huo kutohujumu miundombinu ya miradi inayojengwa na badala yake wasaidie kuimarisha ulinzi  kwa  kujenga uzalendo  zaidi.

Ameyasema hay alipotembelea stendi  ya mabasi ya mji wa Sumbawanga iliyoanza kujengwa mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka 2019 na kutarajiwa kumalizika mwezi Disemba mwaka huu akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Wataaalamu wengine kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Sumbawanga. 

Akitoa taarifa ya ujenzi huo Mhandisi wa Manispaa ya Sumbawanga Suleimani Mziray alisema kuwa kutokana na ufinyu wa fedha stendi hiyo itajengwa kwa awamu mbili na mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 40 na bado mkandarasi anaendelea na ujenzi na kuongeza kuwa katika jengo hilo kutakuwa na eneo la kuwahifadhi abiria zaidi ya 400 watakaokuwa wakisubiri safari zao za nje na ndani ya mkoa.

“Kutokana na Ufinyu wa fedha ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la katumba Azimio utafanyika kwa awamu mbili ambapo mpaka sasa kazi zimekwishafanyika kwa asilimia 40 na bado inaendelea kwenye maeno tofauti kulinngana na Mkataba, jengo Kubwa litakuwa nae neo kwaajili ya kusubiria abiria ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba abiria 400,” Alisema

Aidha Msimamizi wa ujenzi huo kwa upande wa Mkandarasi Said Rajabu Mbelwa ameongeza kuwa ili kufika kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo hilo kutakuwa na Lifti ili kuwasaidia walemavu na wale ambao afya zao haziruhusu kutumia ngazi
“Hapa kuna Lifti ambayo itatumika kwaajili ya Walemavu n ahata ukiwa mgonjwa kwasababu itakuwa siyo rahisi kupita kwenye ngazi ya kupanda kwa mguu kama una matatizo ya afya, kwahiyo imewekwa kwaajili ya walemavu na watu amba afya zao si nzuri sana,” Aliongezea. 

Hadi kufikia hatua hiyo mkandarasi SUMRY ENTERPRISES LTD tayari ameshalipwa Shilingi Bilioni 1.72 ambayo ni sawa na asilimia 28.89 ya Shilingi bilioni 5.95 ambayo ni gaharama ya ujenzi wa stendi hiyo, ambayo inategemewa kuwa na vyumba vya kulala waheni, vymba maalumu vya kufanyia mazoezi(Gym), kituo cha polisi, sehemu ya migahawa mikubwa na mama lishe na sehemu za kuegeshea Baiskeli, Bodaboda, Bajaji, Teksi na mabasi yanayosafirisha abiria ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa. 

0746248872.

Comments