Na Israel Mwaisaka,Nkasi
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kwenda jela miaka 50
Ally kibwe (20) mkazi wa kijji cha Ninde kata ya Ninde wilayani Nkasi
kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa shule ya msingi
Mkilinga wa darasa tano.
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Ramadhani
Rugemalila alidai kuwa mahakama yake imejiridhisha na maelezo ya
upande wa mashitaka na kumkuta na hatia mtuhumiwa na kwenda kutumikia
kifungo jela miaka 50 chini ya kifungu cha 130 (1)(2) (e) ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Jemsi Mlawa aliiambia
mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alimbaka mwanafunzi huyo wa darasa
la Tano kwa nyakati tofauti tofauti na kupelekea kumpa ujauzito
mwanafunzi huyo wa miaka 12.
Aliieleza mahakama hiyo kuwa kitendo cha mtuhumiwa kufanya kitendo
hicho ni kosa kisheria kifungu cha 60 A (3) cha sheria ya elimu sura
ya 353 kama ilivyorekebishwa kwa kifungu cha 22 cha sheria No,4/2016.
Upande wa mashitaka uliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa
ili liwe ni fundisho kwa wengine na ndipo hakimu wa mahakama hiyo
alipotoa adhabu hiyo licha ya utetezi wa upande wa mashitaka kutaka
Mahakama imuhurumie kutokana na kwamba hilo ni kosa lake la kwanza
kulitenda
Comments
Post a Comment