kushoto ni mkuu wa wilaya ya kalambo akiongea na wanufaika wa tasafu |
Na Baraka Lusajo. Kalambo
Mkuu
wa wilaya ya kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura amezitaka kaya masikini
zinazowezeshwa kupitia mfuko wa tasafu kuzitumia vizuri fedha wanazopatiwa na
serikali kwa kuzielekeza zaidi katika shughuri mbalimbali za maendeleo yao
binafusi na kuwasaidia kujikwamua na hali ya kiuchumi.
Binyura
ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo inayofanywa wananufaika wa
mpango wa tasafu katika vijiji vya Jengeni na Safu vilivyopo mpakani mwa nchi
ya Tanzania na Zambia wilayani kalambo mkoani hapa.
Amesema
amelazimika kuanzisha oparesheni ya ukaguzi wa wanufaika wa mradi huo kutokana
na kuwepo kwa malalamiko kwa badhi ya
maeneo kupewa fedha watu ambao sio walengwa
wa mradi huo.
Mratibu wa
mradi tasafu wilayani humo
Michael Mwasumbi amesema fedha hizo
hutolewa kulingana na hali
‘’kwa
mwaka 2019 kaya 4545 katika vijiji 66 vimeingizwa kwenye mpango wa kunusuru
kaya masikini , ambapo kiasi cha shilingi milioni 1,244,000/=zimelipwa katika
kijiji cha Jengeni na kiasi
cha shilingi milioni 1,920,000/=
zimelipwa katika kijiji cha Safu vyote
vinapatikana mpakani mwa nchi ya Tanzania
na Zambia.’’alisema Mwasumbi.
katikati ni mratibu wa tasafu wilayani kalambo akiongea na wanufaika wa mpango wa tasafu |
Baadhi
ya wanufaika wa mfuko huo wilayani humo wamempongeza Raisi wa jamhuri ya
mungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha hizo kwani
zimewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza
maisha yao.
katika picha ni wanufaika wa mpango wa tasafu wilayani kalambo |
Palizoni
Mpinya mnufaika wa mpango wa
tasafu katika kijiji
cha Jengeni amesema
wanampongeza Raisi Magufuli kwa kutoa fedha hizo
kwani zimekuwa msaada mkubwa katika
maisha yao kwa ujumla
hususani katika kusimesha
watoto waao pamoja na kuendeleza miradi mingine.
‘’tunasomesha watoto pia
tunavaa kutokana na miradi ya tasafu, hivyo hatunasababu ya
kumshukuru mh.Raisi kwa
kutangalia sisi wanyonge hususani katika
kutupatia fedha hizi.’’alisema
mnufaika huyo.
Comments
Post a Comment