Na Baraka lusajo- Kalambo.
| KATIKA PICHA NI MWENYEKITI WA CWT KALAMBO |
Watumishi
wa umma wilayani kalambo mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha wafanyakazi wa
serikali walio masomoni kuto pandishwa madaraja licha ya kufuata vigezo na
masharti ya utumishi wa umma wakati wa
kwenda masomoni na kuutaka uongozi wa halmashauri hiyo kutoa ufafanuzi zaidi
juu ya swala hilo kwa lengo la kuondokanana sitofahamu hiyo.
| KATIKA PICHA NI WATUMISHI WILAYANI KALAMBO |
Wilaya
ya kalambo kwa mwaka 2019/2020 imefanikiwa kupandisha madaraja watumishi wapatao
540 huku walimu wakiwa ni 455 na idara
zingine ikiwa ni 85 na huku watumishi wapatao 52 wakibadilishiwa
miundo yao ya kiutumishi.
Wakiongea
kupitia kikao kazi kilichojumuisha watumishi wote wa wauma wilayani humo,wamesema kumekwepo na changamoto ya watumishi waliomasomoni
kutopandishwa madaraja licha ya kwenda
kwa kufuata vigezo vyote.
Dosephu
Ndalama mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani humo, amesema wamekuwa wakipata malalamiko kutoka kwa watumishi
‘’utakuta
mwalimu huyu alipokuwa anaenda
masomoni alifuata taratibu zote
lakini inakuja kushangaza pale wengine wanapopandishwa madaraja lakini wao
wamekuwa wakishindwa
kupandishwa sasa hili
tuanaona sio haki hivyo tungependa kupata ufafanuzi zaidi kuwa kwanini walimu hawa wapati nafasi’’alisema
ndalama.
Aidha
aliipongeza serikali kwa jitihada zinazofanywa
na serikali ya wilaya hiyo hususani za
kupandisha madaraja walimu pamoja
na watumishi wengine wote
kwa ujumla.
‘’tunamkupongeza sana mkurugezi kwa kupandisha madaraja watumnishi na
mpaka sasa kuptia ofisi ya utumishi
tumeambiwa kuwa watumishi wameanza kuchukua barua zao za kupandishwa madaraja
kwa hilo tunakupongeza sana.’’alisema Ndalama.
| KATKA PICHA NI AFISA UTUMISHI -KALAMBO |
| KATIKA PICHA NI MKURUGEZI -KALAMBO |
Afisa
utumishi wilayani humo Amandus Mtani amesema wamepata muongozo mpya kutoka serikalini
unaolezea watumishi waliomasomoni kwa muda mrefu kuto pandindishwa madaraja.
‘’kuna
muongozo mpya tumepewa serikali ambao
unaelezea watumishi waliomasomoni kwa
muda mrefu kuto pandishwa madaraja’’alisema
Mtani.
Mkurugenzi
mtendaji wa hlmashauri ya Wilaya ya hiyo Msongela Mpalela, amewataka watumishi wote kujenga mazoea ya kuchukuliana
katika vituo vyao vya kazi kwa kuishi kwa amani bila migogoro kujitokeza.
‘’niwatake
watumishi wangu jifunzeni kuchukulina hasa watumishi miliko huko ngazi za chin
kwani mkifanya hivyo mtasiwisha
upendo na amani kwenye maeneo
yenu ya kazi pia lazima mkumbuke kuwa si kila siku ni jumapili kiongozi wako anaweza kukukasirisha kutokana
na matatizo ya kifamilia hivyo jifunzeni
kuchukulina’’.alisema Msongera.
| KATIKA PICHA KATIBU TAWALA AKIONGEA NA WATUMISHI |
Katibu
tawala wilayani humo Frank Sichalwe
amewataka watumishi kuacha tabia ya kuruka ngazi hususani wakati wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kutoka kwa viongzi
husika..
Comments
Post a Comment