WANANCHI WAWEKWA KITIMOTO BAADA YA KUGAWANA NYAMA YA TEMBO.


Na baraka  lusajo. Kalambo.

Wananchi katika kijiji cha Kalambo kata ya Mpombwe Tarafa ya Kasanga wilayani kalambo mkoani Rukwa wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamia eneo la hifadhi ya kalambo asilia na kufanya mauaji ya mnyama aina ya tembo kisha kugawana nyama kinyume na utaratibu.

Akithibitha kutokea kwa tukio hilo afisa tarafa ya Matai Endrue Manyema Ngindo amesema watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani  humo baada ya kukamatwa na nyama ya tembo kufuatia msako mkali uliokuwa umefanyika  kijijini hapo kufuatia kutokea kwa tukio hilo.

katika picha ni  afisa tarafa ya kasanga Endrue  Ngindo 
Amesema tukio hilo liligundulika baada ya baadhi ya wanakijiji kuonekana katika maeneo hayo wakigawana nyama na hivyo kupelekea uongozi wa kijiji na kata kutoa taarifa polisi ambao  walifika mapema eneo la tukio na kisha kufanya msako mkali .

‘’watu watano tumewakamata wakiwa na nyara za serikali wa kwanza ni Lucas Mjanlwazira  huyu tulimkamata na nyama ya tembo,wapili ni Joseph mizyuka huyu tulimkamata pia na nyama ya tembo,watatu ni Mejani Sipanje huyu tulimkamata na nyama ya tembo,wa nne ni John Michael huyu pia tulimkamata  na tembo na Jery Simtely huyu pia  tulimkamata na mguu wa digidigi, vichwa viwili  vya ndege,Mfupa mmoja  wa mamba,ganda la moja la risasi  pamoja  na Ngozi ya nyoka.’’alisema Ngindo.

Aidha Ngindo amewataka wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo na hifadhi na kufanya mauaji ya wanyama kwa lengo la kuondokana na matatizo yasiokuwa ya lazima.



Comments