katika picha ni baadhi ya akina mama wa kijiji cha kisungamile |
Na Baraka Lusajo-Kalambo.
Wananchi
katika kijiji cha Kisungamile kata ya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana
na watu wengine dunia kote katika kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji ambayo ufunguzi wake ulifanyika katika eneo la Kisumba Agost moja 2019.
Kama
tunavyofahamu,kuanzia tarehe moja hadi saba Agost,kila mwaka Tanzania huungana na nchi
zingine duniani kote katika kuadhimisha wiki ya uonyeshaji maziwa ya mama.
Madhimisho hayo ni fulsa ya pekee katika kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali
na jamii kwa ujumla ili kiufikia malengo ya azimio la Innocenti ilililofanyika
nchini Italia 1,8,1990.
![]() |
katika picha ni baadhi ya wahudumu wa afya |
Licha
ya hilo kwa ujumla lengo la madhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yamekuwa
yakilenga zaidi kumnyonyesha mtoto maziwa
katika saa moja ya kwanza mara tu baada ya kujifungua sambamba na kumyonyesha mtoto mra kwa mara.
Awali
wakitoa elimu kwa wananchi wahudumu wa afya katika zahanati ya Kisungamile
wamesema uonyonyeshaji ni jukumu la kila
mtu katika nafasi yake ,watu hao ni pamoja na baba ,familia ,viongozi ,ngazi ya
jamii.
Baadhi ya wananchi kijijini hapo wamesema wamenufaika
na elimu iliotolewa na
wahudumu wa afya na
kuiomba serikali na mashirika
binafus kuendelea kutoa
elimu zaidi juu ya namna ya
unyonyeshaji.
Hata
hivyo siku za hivi karibuni mkuu wa mkoa
wa Rukwa Joachim Wangabo alivitaka vyombo vya
habari mkoani humo kufuatilia na
kufanya tafiti na kuripoti
juu matukiio mbalimbali ikiwemo haki ya akina mama kupata likizo ya
uzazi sambamba na kuandika taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji.
Comments
Post a Comment