Na Baraka Lusajo. Rukwa.
Ziara ya mafunzo ya wahasibu themanini kutoka kanda nane za
wakala wa huduma za misitu nchini-TFS- ya kuyatembelea maporomoko
ya maji ya kalambo yaliyopo
wilayani kalambo mkoa
wa Rukwa imetoa
elimu ya jinsi ya kuyatumia maporomoko hayo kwa faida za kiuchumi wa taifa.
| Katika picha ni mkurugezi mtendaji wa hlmashauri ya kalambo Palera Msongela baada ya kutembelea maporomoko ya kalambo fall na watalii kutoka nchini swaziland. |
Mhasibu mkuu wa TFS makao makuu Peter Mwakosya amesema maporomoko
ya Kalambo yanayoshika
nafasi ya pili kwa urefu barani Afrika hayajatumika kikamilifu
kwa ajili ya manufaa ya taifa licha ya kuwa kivutio cha kupendeza kwa watalii
wa ndani na nje
Amesema wakati umefika kwa serikali kushirikiana na wadau mbalimbali
katika sekta ya utalii kuboresha miundo mbinu rafiki kwa ajili ya utalii ili
kusaidia kukuza pato la taifa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ya jamii.
Msaidizi mkuu wa meneja wa TFS kanda ya nyanda
za juu kusini Innoncent lupembe amesema hivi sasa zimefanyika
taratibu za kushirikiana na mamlaka husika za utalii nchini Zambia ili kwa pamoja kuyatumia
maporomoko ya kalambo kwa
faida .
Josephat Chezue meneja wa wakala wa hifadhi za misutu wilayani
kalambo amesema mpaka sasa wanaendelea
na ujenzi wa
nyumba za kufikia wageni
pamoja na ngazi za kupandia kutoka juu hadi chini na kuwataka
watalii wa ndani na nje kuendelea kutembelea maeneo hayo.
ziara ya mafunzo ya wahasibu kutoka kanda zote za TFS nchini
inatarajiwa kuja na ufumbuzi sahihi wa matumizi sahihi yenye faida ya
maporomoko ya Kalambo
Comments
Post a Comment