Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 24.08.2019: Neymar, Mustafi, Van Dijk, Sanchez, Dybala, Pjanic

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali ya mchezaji huyo kujeruhiwa mara kwa mara. (Marca - in Spanish)
Lakini ripoti zinaarifu kuwa Real na mahsimu wao Barcelona wanahoji masharti ya malipo ya hali ya juu yanayodaiwa na Neymar. (AS - Spanish),
Baba mzazi wa na wakala wa beki wa Arsenal wa miaka 27-Shkodran Mustafi wanasema mchezaji huyo raia wa Ujerumani ana mpango wa kuhama klabu hiyo. (Mirror)
Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, 28, anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya na klabu hiyo ambayo itaongeza mara mbili malipo ya mchezaji huto wa raia wa Uholanzi hadi £250,000 kwa wiki. (90min).
Manchester United wana matumaini ya kumuuza mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 30, kabla dirisha la usajili wa wachezaji barani ulaya kufungwa. (Mirror)
Wachezaji wa United wanataka mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 21, awe akipiga mikwaju ya penalti baada ya mkwaju wa penalti wa Paul Pogba kushikwa wakati wa mechi yao dhidi ya Wolves. (Mail),
Tottenham wanatafakari kumuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, wakipokea dau la angalau £50m. (Mail).
Winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane, 23, huenda akarejea uwanjani msimu huu baada ya kuumia goti wakati wa michuano ya Community Shield mapema mwezi Agosti. (Sun)

Bayern Munich wanajiandaa kujaza pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Ureno Renato Sanches,aliyejinga na Lille, kiungo wa kati wa Espanyol Mhispania Marc Roca anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo. (L'Equipe - in French),
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane haamini kipa wake Keylor Navas, 32, ataondoka klabu hiyo licha ya tetesi zinazomhusisha na Paris St-Germain.(Marca)
Crystal Palace wanashauriana na mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28 kuhusu mkataba mpya. (Evening Standard)
Tottenham huenda wakapata nafasi ya kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala, 25, mwezi Januari ikiwa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina atasalia Juventus. (Football.London).
uve wanasemakana kuvutiwa na wazo la kiungo wa kati Miralem Pjanic, 29, raia wa Bosnia kuondoka klabu hiyo msimu huu wa uhamisho wa wachezaji.(calciomercato)

Tetesi Bora Ijumaa

Ujumbe wa wawakilishi wa Real Madrid upo Ufaransa kufanya majadiliano juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27 kutoka klabu ya Paris St-Germain. (Marca - in Spanish)
Barcelona wamekataa ofa ya klabu ya Inter Milan ambao wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal, 32, kwa mkopo. (Mundo Deportivo)Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28, na mlinzi raia wa England James Tomkins, 30, wapo katika mazungumzo ya kuongeza mikataba yao na klabu ya Crystal Palace. (Guardian)
Winga raia wa Brazil anayekipiga na klabu ya Chelsea Kenedy, 23, anaangalia uwezekano wa kuihama moja kwa moja klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la ulaya kufungwa wiki ijayo. (Goal)
Miamba ya Uturuki klabu ya Fenerbahce imejitenga na harakati za uhamisho wa beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 29. (Star).


Comments