Na Baraka Lusajo-Rukwa.
Serikali mkoani Rukwa
imesema ina ziada ya chakula 470,793.6
baada ya msimu wa mavuno wa mwaka 2019, 2020 kufanikiwa kuvuna tani 884,368.8 ikiwa ni sawa na asilimia 69 ya
mavuno yote na kusisitiza wananchi kuendelea kulima mazao kwa kushirikina na
wataalamu.
Mkuu wa mkoa huo
Joachim Wangabo jana alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake wakati akiwatoa hofu wananchi wa mkoa huo kuhusiana na kuwepo kwa
tishio la upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Alisema kuwa mkoa wa
Rukwa unatarajia kutumia tani 413,575 kwa mwaka 2019,2020 na kubakiwa na ziada
hiyo ya chakula hivyo mkoa huo unachakula cha kutosha na hakuna hofu yoyote
katika hilo.
Wangabo alisema kuwa
hata hivyo uzalishaji umeshuka kwani mkoa ulitarajia kupata chakula tani
1,677,474.8 lakini ulipata tani 1,164,242.42 hata hivyo pamoja na kutofikia
lengo la uzalishaji kwa asilimia mia moja lakini bado kuna ziada hiyo ya
chakula.
Alisema kuwa tayari
serikali kupitia wakala wa hifadhi ya chakula(NFRA) imetoa fedha kwaajili ya
kununua tani 18,000 ya chakula ambapo mkoa wa Rukwa itanunua tani 13,000 na
katika mkoa wa Katavi itanunua tani 5,000 kwaajili ya kuhifadhi.
‘’katika msimu wa ununuzi wa 2019/2020 wakala wa hifadhi ya chala na cha taifa kanda ya sumbwanga umepangiwa kununua mahindi kiasi cha tani 18,000 kati ya hizo tani 13,000 ni kwamkoa wa Rukwa na ununuzi utafanyika Namanyere kwa wilaya ya Nkasi,Mwimbi na Matai kwa wilaya ya Kalambo ,mazwi ,mtowisa na laela kwa wilaya ya Sumbawanga’’alisema wangabo.
Naye Richard Luah
afisa ugavi wa NFRA mkoa wa Rukwa alisema kuwa mwaka huu serikali itanunua kilo
moja shilingi 500 ambapo gunia la kilogramu 100 litanunulia kwa shilingi 50,000
bei ambayo itakuwa nzuri tofauti na walanguzi ambao wamekuwa wakiwalalia
wakulima na kununua gunia hilo hadi shilingi 18,000.
katika mpicha ni afisa ugavi NFRA mkoani Rukwa Naye Richard. |
Aliwaomba wakulima
kuhakikisha wanazingatia ubora wa mazao hayo kwa kuwasafisha na kuyakausha
vizuri sambamba na kuacha tabia ya kuchanganya na uchafu mwingine ili yawe
mazito kwani wanaweza wasifanikiwe kuyauza mazao hayo hususani mahindi kutokana
na kushindwa kukidhi ubora.
Aliwasihi wakulima kuhakikisha kuwa wanauza mazao yao mapema
ili wapate fedha kwaajili ya kuanza kununua pembejeo za kilimo kwaajili ya
msimu ujao kwani wakiiacha fursa hiyo watauza mazao yao kwa bei mbaya na
matokeo yake watashashindwa kufanya vizuri katika msimu ujao wa kilimo.
wasilina nasi kwa 0746248872.
Comments
Post a Comment