Na Baraka lusajo.Rukwa-kalambo
Katika Picha ni mkuu wa mkoa Wa Rukwa akiongea na wanahabari ofini kwake |
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewataka wataalamu wa afya mkoani humo kuendelea
kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu
wa unyonyeshaji kwa akina mama wote kwa lengo la kusaidia kupata watoto wenye
ulewa na afya nzuri.
Wiki
ya unyonyeshaji hufanyika kuanzia tarehe moja ya kuanzia agosti moja hadi saba kila
mwaka,ambapo kwa mwaka 2019 madhimisho hayo kimkoa yatafanyika katika kata ya
kisusumba wilayani kalambo na huku kauli mbiu ikiwa ni ‘’mwezeshe mama aweze
kunyonyesha’’
Akiongea
na kituo hiki ofisini kwake mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo amesema lengo la
serikali ni kuhakikisha jamii inapata uelewa kuhusu jinsi,usawa wa
kijinsia,sheria na kanuni zinavyowezesha kulinda ,kuendeleza na kusaidia
uonyeshaji maziwa ya mama ili kuboresha
lishe ya watoto na jamii.
‘’unyonyeshaji
ni jukumu la kila mtu katika nafasi yake,watu hao ni pamoja na baba,familia,viongozi
ngazi ya jaamii,wafaanyakazi wa afya wenye ujuzi,wataalamu wa masuala ya uonyonyeshaji na marafiki , pia ni vizuri kwa mama kupata
muda na msaada wa kutosha katika kipindi cha kunyonyesha na pia apate elimu ya makuzi na malezi
kwa watoto wake’’alisema Wangabo.
Alisema
licha ya hilo vyombo vya habari vinaweza kufuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali zinazolinda haki za uzazi
na uzalishaji wa watoto kwa kufanya
tafiti ,kuandika,kuripoti matukio mbalimbali ikiwemo haki ya kupata likizo ya uzazi.
Kaimu
afisa lishe mkoani humo Asha Izina, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha
akina mama wote wanapewa kipaumbele zaidi
hususani wakati wa kipindi cha
unyonyeshaji kwa lengo la kusaidia kuondokana na adha ya udumavu
kwa watoto
Madhimisho
ya wiki ya unyonyeshaji yatafanyika sambamba na siku ya afya ya kijiji yatakayo
fanyika katika vijiji vyote kuanzia agost moja 2019 katika kijiji cha Kisumbakati wilayani
kalambo mkoani hapa.
Asante kazi nzuri cha msingi wataramu watimize wajibu wao
ReplyDelete