Morogoro: Tamko la Rais Magufuli kuhusu ajali ya lori la mafuta Tanzania

Rais wa Tanzania John MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU TANZANIA
Rais wa Tanzania, John Magufuli amepokea amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 60 na wengine 70 kujeruhiwa vibaya baada yakuungua kwa moto baada ya lori lililokuwa na shehena ya mafuta kupata ajali na kisha kulipuka moto Mjini Morogoro.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wote waliopoteza jamaa zao
katika ajali hiyo na pia amewaombea majeruhi wapone haraka,
Taarifa rasmiHaki miliki ya pichaIKULU TANZANIA
Taarifa hiyo pia imekemea vitendo vya wananchi wanaovamia magari yenye milipuko akitaka vikomeshwe mara moja.
Ajali hiyo ilitokea mapema Jumamosi mwendo wa saa mbili asubuhi wakati ambapo lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva
wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.
"Nimeumia sana kusikia idadi kubwa ya Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, natoa pole kwa wote walioguswa na vifo hivi hasa familia za marehemu wote, nawaombea marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka" amesema Rais Magufuli.
Watu waliokusanyika karibu na eneo la tukioHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu waliokusanyika karibu na eneo la tukio Morogoro
"Baadhi ya magari haya yanabeba mafuta ambayo ni hatari kama ilivyotokea Morogoro, yapo magari yanabeba kemikali za sumu, yapo magari yanabeba milipuko nakadhalika, nawaomba sana tuache tabia hii," amesisitiza kiongozi huyo mkuu
Taarifa hiyo pia imesema, Rais Magufuli amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe kufikisha salamu zake za pole kwa familia na wote walioguswa na vifo hivyo.
"Rais Magufuli ameagiza wizara zote zinazohusika kushughulikia ajali hii na ametaka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhakikisha majeruhi wote wanapatiwa matibabu ili kuokoa maisha yao," ilisema taarifa hiyo
Si mara ya kwanza visa vya moto inayotokana na malori yaliobeba shehena ya mafuta kutokea katika enao la Afrika Mashariki na Kati.
Mwaka 2010 watu 292 walifariki dunia nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya na miaka mitano baadae watu 203 wakafarikiki nchini Sudan Kusini.

Comments