Mjadala waibuka baada ya ndege ya Air Tanzania kuzuliwa Afrika Kusini

Ndege ya Air TanzaniaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hatua ya Mahakama kuu ya nchini Afrika Kusini kuzuilia kuruka ndege ya Air Tanzania imeendelea kuzua mjadala kuhusu chanzo chake.
Mpaka sasa Mamlaka nchini Afrika Kusini haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo.
Lakini Kwa mujibu wa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ndege hiyo imezuiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya mjini Johannesburg.
Ripo ya vyombo vya habari nchini Tanzania zinaashiria kuwa abiria wote waliokuwa ndani ya Msemaji wa mkuu wa serikali ya Tanzania amesema wanasheria wa wa nchi hiyo wamewasili nchini Afrika Kusini kufuatilia suala hilo na kwamba wakikamilisha mchakato huo watatoa taarifa kamili.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam.
Kufuataia hatua hiyo Air Tanzania imetoa taarifa rasmi kupitia mtandao wake wa Twitter kuwaomba radhi wateja wake na kuongeza kwamba kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake itafanyia marekebisho safari zake
Taarifa iliyotolewa Ijumaa usiku na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Leonard Chamuriho ilieleza kuwa serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu inafuatilia suala hilo.
Taarifa ya serikali

Comments