Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda amepanga kuzisajiri ndoa zote za mkoa huo kwa ajili ya kukabiliana na wanaume wanaowalaghai wanawake kimapenzi.
Bwana Makonda amesema kuna mpango wa kuanzisha kanzi data ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.
Kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa.
Makonda amesema pamoja na kanzidata hiyo atatumia mkutano wa SADC kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo
Mkuu huyo wa mkoa amesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanawake kuumizwa hivyo wakati umefika wa kuanza kushughulikia.
Mkakati wake ameutangaza
Comments
Post a Comment