BARAZA LA MADIWANI NKASI LA MKATAA MKAGUZI WA NDANI.


Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa limeiomba mamlaka yenye dhamana ya ajira kumwondoa kwenye orodha ya watumishi wa halmashauri hiyo mkaguzi wa ndani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
Mwenyekiti wa baraza hilo sumuni mwanakulya amesema uamuzi huo umetolewa kwenye kikao cha robo ya nne ya mwaka cha  kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya kata ishiirini na nane za halmashauri hiyo na kumtuhumu mkaguzi Joseph Sengerema kuzuia fedha za miradi ya maendeleo kutopelekwa  kwenye vijiji na kata.
Kupiotia  kikao  hicho  cha baraza baadhi ya madiwani wamemtuhumu mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo Joseph Sengerema kushindwa kumshauri vizuri mkurugenzi wa halmashauri kuhusu fedha za miradi ya maendeleo na pia  kujenga chuki kati ya wataalamu na madiwani.

kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi  mhandisi Emmanuel sekwao na katibu tawala wa wilaya hiyo cosmas kuyela  wamesema tuhuma zilizotolewa dhidi ya mkaguzi wa ndani zinafanyiwa uchunguzi kabla ya kupelekwa kwenye  mamlaka za maamuzi.

Imedaiwa katika kikao hicho cha madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi kuwa  viporo vya majengo ya vyumba vya madarasa na zahanati zaidi ya elfu moja mia nne katika baadhi ya vijiji tisini  vya halmashauri hiyo hayajakamilishwa kwa kukosa fedha.

Comments