Ligi ya mabingwa Caf: Yanga yafuzu Simba yaondolewa na UD Songo ya Msumbiji

Je mabingwa hao watafanikiwa kupeperusha bendera ya TanzaniaHaki miliki ya pichaMAHMOUD BIN ZUBEIRY
Mabingwa wa ligi ya soka nchini Tanzania Simba wameondolewa katika mashindano hayo baada ya wageni kutoka Msumbiji kujipatia bao moja la ugenini.
Penalti ya dakika za lala salama iliopigwa na Erasto Nyoni haikutosha kuisaidia timu hiyo ya Msimbazi Reds huku Songo ikifuzu katika raundi ya pili kutokana na goli la ugenini.
Luiz Misquissone aliifungia UD Songo katika kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo alicheka na wavu kunako dakika ya 14 na timu hiyo ya Tanzania ilishindwa kusawazisha hadi dakika za mwisho - bao ambalo halikuweza kuwasaidia.
Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems alifanya mabadiliko katika dakika ya 41 akimtoa kiungo wa kati wa Kenya Francis kahata na kumuingiza Hassan Dilunga.
Hatahivyo mabadiliko hayo hayakuleta usaidizi kwa mabingwa hao wa Tanzania.
Timu hizo mbili zilikuwa zimetoka sare tasa katika awamu ya kwanza ya michuano hiyo iliochezwa Msumbiji.

Yanga yafuzu

Wakati huohuo wapinzani wakubwa wa mabingwa hao nchini Tanzania Yanga SC wamefuzu katika raundi ya pili baada ya kupata ushindi muhimu ugenini siku ya Jumamosi.
Yanga SC wametinga raundi ya pili ya ligi ya mabingwa ya Caf baada ya kuilaza Township Rollers ya Botwana 1-0.
Goli la dakika ya 42 lililofungwa na Juma Balinya ndio lililohitajika na mabingwa hao wa Afrika mashariki kuwalaza wenyeji wao na kusonga mbele katika raundi ya pili kwa jumla ya magoli 2-1.
Kufuatia sare ya 1-1 katika mechi ya awamu ya kwanza iliochezwa nchini Tanzania klabu hiyo ya Botswana ilikuwa na fursa nzuri ya kusonga mbele kwani walihitaji sare tasa kufuzu.
Klabu za Simba na Yanga ndio tegemeo Tanzania
Kwa upande wa Yanga walilazimika kufunga goli ili kuimarisha matumaini yoyote ya kufuzu katika raundi ya pili.
Licha ya kipindi cha kwanza kilichosisimua , hakuna timu ilioona lango la mwengine , lakini walikuwa wenyeji waliokuwa na presha ya kupata ushindi.
Yanga sasa itakabiliana na mshindi kati ya Zesco United ya Zambia, ambao walisonga mbele kwa kuilaza Green Mamba 3-0 kwa jumla ya magoli.

John Bocco ni miongoni ma wachezaji wanaotegemewa kuisaidi SimbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Comments