Korea Kaskazini yarusha makombora zaidi wakati Korea Kusini ikifanya mazoezi na Marekani


A ballistic missile being launched from an unknown location in North Korea early on WednesdayHaki miliki ya pichaAFP
Korea Kaskazini imerusha makombora mawili yasiyojulikana, na kufanya idadi ya makombora yaliyorushwa kufikia manne chini ya kipindi cha wiki mbili.
Kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini, makombora hayo yalirushwa kutoka jimbo la kusini la Hwanghae.
Upande wa Kaskazini umeeleza kukerwa kwake baada ya Marekani kuanza mazoezi ya kivita na Kusini jana Jumatatu.
Kaskazini inasema mazoezi hayo yanaenda kinyume na makubaliano waliyofikia na raisi wa Marekani Donald Trump na wa Korea Kusini Moon Jae-in.
Japo mazoezi hasa ya kivita yataanza Agosti 11, maandalizi ya awali yanaendelea.
Marekani imeeleza kuwa inaendelea kupiga jicho juu ya kile kinachoendelea huku ikiwasiliana na Korea Kusini na Japani.
Jumatatu jioni, Washington ilianzisha utaratibu mpya wa kuwabana watu walioyembelea Korea ya Kaskazini kuingia Marekani.
Raia yeyote wa kigeni ambaye alikuwa halazimiki kuomba viza kuingia Marekani hivi sasa itamlazimu kuomba viza iwapo alitembelea Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka nane iliyopita.
Utaratibu huo mpya utawaathiri watalii kutoka mataifa ya Ulaya pamoja na Australia, New Zealand, na baadhi ya nchi za bara Asia kama Japani, Taiwani na Singapore.
An Apache helicopter takes off from US base Camp Humphreys in Pyeongtaek, south of Seoul, South Korea, 5 August 2019Haki miliki ya pichaEPA
Image captionHelikopta za Marekani pia zinahusika katika mazoezi ya kivita Korea Kusini
Kwa nini Korea Kaskazini inajaribu makombora?
Taarifa ya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini inaeleza kuwa ushirikiano wa kijeshi baina ya Kusini na Marekani unawalazimu kuendelea kufanya ugunduzi na majaribio ya silaha mpya.
"Tunalazimika kuendelea, kujaribu na kutumia makombora mazito ambayo ni muhimu kwa kujilinda," imeeleza taarifa ya Kaskazini.
Taarrifa hiyo pia imeeleza kuwa kinachoendelea baina ya Marekani na Korea ya Kusini ni uvunjwaji wa wazi wa mazungumzo ya hivi karibuni baina ya Marekani na Korea Kaskazini (DPRK).
"Tumeshaonya mara kadhaa kuwa mazoezi ya kivita yatazorotesha mahusiano baina ya Marekani na Korea Kaskazini na mahusiano ya Korea zote mbili kwa ujumlana kutufanya tufikirie kurejea tena hatua zetu za awali," inaeleza taarifa ya Kakazini.
Kwa mujibu wa jeshi la Kusini, makombora yaliyorushwa leo jumanne ni ya masafa mafupi yanayoenda mpaka kilomita 450.
Ndani ya wiki mbili zilizopita, Kaskazini imekuwa ikirusha aina mpya ya makombora ya masafa mafupi. Ijumaa iliyopita ilirusha makombora mawili yaliyoangukia kwenye bahari ya Japani.
How could war with North Korea unfold?
Jumatano, Kaskazini pia ilirusha makombora mawili yaliyoenda umbali wa kilomita 250 na kufikia urefu wa kilomita 30 kabla ya kutua katika bahari ya Japani pia.
Julai 25 Kakazini ilirusha makombora mawili na moja likaenda umbali wa kilomita 690, kombora hilo lilirushwa siku chache baada Trump kukutana na kiongozi wa Kaskazini Kim Jong-un kwenye mpaka baina ya kUsini na Kaskazini ambapo walikubaliana kuendeleza mazungumzo ya kuiwezesha Kaskazini kuachana na mipango yake ya silaha za nyuklia.

Comments