Hail Satan?: Filamu ya waabudu shetani wanaopigania uhuru wa kidini

Kila kitu unachokijua kuhusu Ushetani ni uwongo.
Hayo ni kwa mujibu wa filamu mpya inayoangazia Hekalu la Kishetani.
Licha ya ukaribu wa majina, Hekalu hilo ni tofauti na Kanisa la shetani, lililobuniwa mwaka 1966 kupitia msanii maarufu Anton Levey mjini San Francisco, California
Sadaka ya binadamu? Ni vibaya. Kunywa damu? Ni vibya. Ibada ya weusi? Nadhani ni sawa.
Hekalu hilo lilibuniwa mwaka 2013 kwa lengo la "kuhamasisha ukarimu na huruma kati ya watu wote, kupinga mamlaka ya kidhalimu, kutetea fikra na haki ya kawaida, na kuelekezwa na dhamiri ya kibinadamu kufanya shughuli nzuri zinazoongozwa na dhamira ya mtu binafsi''.
Filamu hiyo inahoji wazo la Kanisa kupewa mahali pa kuweka sanamu ya Yesu katika jengo la Capitol katika mji wa Oklahoma.
Mpango wa Hekalu hilo ni kuulizia nafasi ya kuweka sanamu ya mungu wa Shetani kwa lengo la kushinikiza usawa wa kidini duniani, wakati wote huo wakihubiri mafundisho ya kuunga mkono haki ya kijamii na haki za binadamu.
"Tunataka watu watathmini ikiwa wanataka Marekani kuwa taifa la Kikristo,"msemaji wa Hekalu hilo Lucien Greaves anasema katika tela ya filamu hiyo. "Sio Kweli".
"Nilisikia kuhusu Hekalu la Shetani walipokua wakiendesha kampeini yao Oklahoma," anasema Lane.
"Nilidhani wanafanya mzaha kuwa wao ni wafuasi wa shetani na wakati huo walikuwa wanachma 50,000 .
"Kadri nilivyowazia suala hilo ndivyo nilichanganyikiwa na hamu ya kujiunga nao 
Hail Satan? iliongozwa na mtayarishaji filamu wa Marekani Penny Lane, inafuatilia jaribio la Hekalu hilo kudhibiti umaarufu wa dini ya Kikristo katika maisha ya Wamarekani na jinsi dini hiyo inavyoendelea kupata umaarufu wa kisiasa.
Filamu hiyo inamuonesha Greaves na wafuasi wennzake wa shetani wakiwahimiza watu kutoa damu, kukusanya nguo kwa ajili ya kuwasaidia watu wasio na makazi, kusafisha fukwe za umma na kutoa mafundisho kwa watoto wa shule kuhusu maadili ya Hekalu la shetani na malengo yake ambayo ni pamoja na:
  • Mtu kujitahidi kutenda mema na kuwa na moyo wa huruma kwa viumbe vyote kulingana na muongozo uliowekwa.
  • Mtu akifanya kosa ajitahidi kurekebisha kosa hilo na kutatua shida yoyote ambayo huenda imetokana na kosa hilo.
Japo filamu zao ni za kuogofya wakiangazia misa yao inayoonesha picha za shetani, hakuna mfuasi wa Hekalu la Shetani anayeamini nguvu za Shetani.
Misa ya kundi hilo ni ya kutisha na huendeshwa kwa mfumo wa sanaa ya kuigiza
"Si kuona ugumu wa kujifunza namna ya kuomba," anasema Lane.
"Si ajabu kwa sababu mafundisho ya dini huendeshwa kwa misingi ya imani lakini sio dhahiri.
"Nilielewa kuwa mtu hahitaji kuamini kitu ili kuelewa umuhimu wake. Nadhani haki ya binadamu ni muhimu na ningelipendelea kuzilinda kwa niaba ya watu wengine, lakini siamini uhalisia na uwepo wa haki za binadamu duniani.
"Kwa mfano vitu vyote ambavyo wanadamu wanaamini ni muhimu kama vile upendo haki na uhuru ni dhana tu. Vitu hivi vinaonekana kama wazo tu lililobuniwa."
apo filamu hiyo inaangazia zaidi juhudi ya Hekalu hilo kuweka sanamu ya ''mungu wao'' katika miji mikuu ya Marekani, pia inagusia "hofu ya Shetani" wimbi la hofu ya kimaadili lililoteka Marekani miaka ya 80 na 90 -lililoendeshwa kupitia muziki na michezo ya video na bao- la Dungeon na Dragon.
Waumini wa Kikikristo wenye misimamo mikali na mamlaka nchini ziliona mfano wa uabudu wa shetani kila mahali.
Ni kipindi hicho cha miaka 10 hadi 15, ambapo kulikuwa na wazo la kimsingi la kupangwa kwa njama za siri za Shetani ambapo watu walikuwa wakifanya mambo mabaya kama mauaji na kutesa wanyama na kubaka watoto kwa kujifanya shetani.
"Ukifanya utafiti kuhusu suala hilo, huenda ukabaini hakuna waabudu shetani,na wala hapakuwa na siri zilizofichwa chini ya ardhi. Kama anavyosema Lucien katika filamu hii, aligundua kuwa uovu halisi unapatikana katika kitendo cha kuhujumiana.
Na hili ni jambo ambalo tunastahili kujua kuwa linaweza kufanyika katika jamii.
"Hakuna mtu aliyejaribu kukubaliana na matukio ya zama hizo kwa mfano kilichofanyika na kilichotokea hadi msimu huo ulipokamilika. Nadhani Hekalu la Shetani linataka watu wakumbuke zama hizo na kujua kilichofanyika wakati huo."
Greaves (sio jina lake halisi, anatumia majina tofauti kulinda familia yake) ametishiwa maisha mara kadhaa wakati wa kampeini ya kundi hilo na amekuwa akivalia jaketi ya kuzuia risasi kupita wakati sanamu yake ikiziduliwa.
"Ni wazi kuwa anatilia maanani wazo la kulinda familia yake isitambulike," anasema Lane.
Kuna watu wengi sana ambao wanafuraihia kuihangaisha familia yake bila sababu ya kimsingi.
"Nilijihofia mimi binafsi na usalama wa watu wote walioigiza katika filamu hiyo.
Bila shaka walipokubali kuigiza filamu hii walijiweka hatarini kote duniani. Nafahamu fika kuhusiana na hilo," Lane alisema.
Cha kushangaza nikuwa yeye sio mwanachama wa Hekalu la Shetani lakini wanaomjali Lane wanajumuika naye bila tatizo lolote.
"Ukweli ni kwamba wa kidini wamenichanganya sana maishani," aliongeza.
"Najua tamko langu linaeleweka vibaya lakini ukwili wa mambo ni kwamba,binafsi nawachukulia waumini wa kidini kama watu walio na akili punguani na wanahitaji kutibiwa''
Filamu ya Hail Satan? inapatikana katika kumbi za sinema na imekuwa ikiwavutia watu wengi tangu Agosti 23.

Comments