Mwandishi habari Tanzania Erick Kabendera amepandishwa kizimbani kusomewa mashtaka mapya matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi .

Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu na uchumi nchini kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania.
Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.
- 'Walinihoji kwa zaidi ya saa 10 mbona wasiweke kumbukumbu' ?
- 'Kwa nini tulimkamata Kabendera'
- Idara ya uhamiaji yasema inamhoji Kabendera
Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiawa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani leo.
Makosa yote hayana dhamana.

Mawakili wake wameondoa ombi la dhamana kutokana na mashtaka hayo mapya.
Akizungumza na wanadishi habari punde baada ya Kabendera kusomewa mashtaka, wakili wake Jebra Kambole amesema
'Wakati Erick anakamatwa siku ya kwanza aliambiwa kosa lake ni la uhamiaji, akapelekwa kwenye mamlaka za uhamiaji, akahojiwa, pasipoti yake ikachukuliwa. Uhamiaji wakamkabidhi kwa jeshi la polisi makao makuu Central Jeshi la Polisi wakamhoji kwa makosa ya uchochezi.
'Kuanzia hapo hajawahi kuhojiwa kwa makosa mengine zaidi ya hayo' amesema Jebra Kambole.
Amefafanuwa kwamba kutokana na kwamba mashtaka aliyosomewa Kabendera hayana, ameshindwa kutoka leo.
Chanzo cha habri bbc swahili.
Comments
Post a Comment