katika picha ni mkurugezi mtendaji wa halmashauri ya kalambo Msongera palela |
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kalambo Mkoani Rukwa Msongera Palela amezitaka Asasi zinazotekeleza miradi mbalimbali wilayani
humo kukemea na kupinga mira potofu za wanawake kupakwa unga kichwani na
kuwekewa sherehe kubwa pindi wanapokuwa wamepewa ujauzito kwa madai ya kuwa ni
mashujaa.
Msongera
ameyasema hayo wakati
wa uzinduzi wa mradi wa ukatili wa
kijinsia unaotekelezwa na Asasi ya Sucoda,ambapo amesema baadhi ya mira
wilayani humo zimekuwa zikiendekezwa na wananchi husani kwenye maeneo ya vijijini bila kujua athari zake.
Amesema
kitendo cha wanawake kupakwa unga kichjwani pindi wapatapo ujauzito ni kitendo cha
kibaya kwani kinahamasisha mimba za utotoni .
‘’anapopata
ujauzito anashangiliwa kuwa yeye ni shujaa, sasa mira hizi ni potofu na
ukizitazama mira kama hizi utakuta zinaendekeza mimba za utotoni ‘’alisema
Msongera.
Katika picha ni mwenyekiti wa halmashauri yaa kalambo akiongea na watumishi wa uma. |
Amesema
licha ya hilo mira hizo zimekuwa zikipelekea kujitokeza kwa vitendo vya utoro
mashuleni kitu ambacho ni hatari kwa
wanafunzi kuendelea na masomo hususani wa kike.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Daudi Sichone,amesema asasi zote hazinabudi kuungana na
viongozi wa serikali za vijiji kwa kutoa
mafuzo ambayo yatasaidia wao kuwaelimisha wananchi wao pindi wanakuwa kwenye mikutano ya hadhara.
katika picha ni mwezeshaji wa mafunzo ya ukatili wa kijinsiaVastina Valeli. |
‘’hatuwezi
kurudi nyuma kimsisingi sisi kama halmashauri ya wilaya tuna jukumu la
kuwasaidia wananchi kuondokana na
chagamoto zinazowakabili.’’alisema sichone.
Vastina
Valeli mwezeshaji wa mafunzo ya
ukatili wa kijinsia
amesema lengo ni kuhakikisha
matukio ya ukatili wa kijinsia yanatokomezwa na kusaidia kuwajengea uwezo wakuu
wa idara na watumishi wengine.
katika picha ni mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura akiongea na watumishi wa uma. |
Mkuu
wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amewataka wananchi kushirikina na dawati
la ukatili wa kinsia katika kutoa
taarifa sahihi juu ya uwepo wa matukio hayo ambayo yamekuwa yakikwamisha maendeleo katika
jamii zao husika.
Comments
Post a Comment