DC- SONGWE ASISITIZA AMANI KATIKA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA,ASEMA ATAKAYELETA FUJO ATAKIONA CHA MTEMA KUNI.


Na Ibrahim Yassin,Songwe


WATAKAOLETA fujo katika harakati za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi wa 11 mwaka huu,watakiona cha mtema kuni kwani kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuhakikisha jeshi la polisi linasimama imara katika kata zote 18 ili uchaguzi ufanyike wa uhuru na haki.
Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Songwe mkoani hapa,Samwel Jeremiah wakati akizungumza na watendaji na madiwani wa halmashauri hiyo katika kikao cha kawaida cha robo ya 4 kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Jeremiah,alisema ni lazima amani iliyopo idumishwe na kuwataka viongozi wa kamati za siasa za vyama vya siasa kuondokana na propaganda za upotoshaji,rugha za kuudhi,matusi n a mambo mengine yasiyofaa huku akiwatahadharisha wanasiasa watakaokiuka agizo hilo watakiona cha mtema kuni.
Hata hivyo katika kuhakikisha amani iliyopo inaendelea kudumishwa,Dc,Jeremiah,alizitaka kamati za siasa za kata ambazo diwani ni mwenyekiti katibu wake akiwa ni mtendaji kata kuhakikisha wanakaa kila mwezi kujadili hali ya usalama katika kata zao.
‘’Kila kata kupitia kamati zao za ulinzi zihakikishe zinakaa kujadili hali ya usalama,na pale wanapoona pana viashiria vya uvunjifu wa amani watoe taarifa kupitia askari kata kwani jeshi la polisi limeweka askari mmoja mmoja kila kata kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao’’alisema.
Aliongeza kuwa katika vikao hivyo,pia wanatakiwa kujadili na kuitatua migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ni tatizo kubwa katika wilaya hiyo na kwamba kwa sasa serikali imejipanga kuhakikisha inatokomeza migogoro hiyo na kulinda amani iliyopo.
Abraham Sambila,mwenyekiti wa halmashauri hiyo,alisema hoja ya mkuu wa wilaya inamashiko na kwamba kwaniaba ya madiwani watahakikisha vikao vinakaliwa kuhakikisha amani na usalama uliopo unaendelea kulindwa ili wananchi waendelee kuifurahia serikali yao.
Philipo Mulugo,Mbunge wa jimbo la Songwe,alisema iwapo viongozi wa kata watatii agizo hilo,anauhakika usalama uliopo utaendelea kuimarika na kwamba kuelekea uchaguzi ujao wanategemea kamati ya ulinzi na usalama itaimarisha usalama na uchaguzi utafanyika pasipo fujo za aina yeyote.
‘’Wilaya ni kubwa inamapori mengi,mifugo mingi inaingia halmashauri katika mwaka wa fedha 2020 imetenga fedha kwa ajili ya kujenga Rambo na Majosho kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji kwani sheria nyingi za vijiji tunatumia za wilaya ya Chunya,watendaji waache kuzidisha faini kwa wafugaji’’alisema.
Mwisho.

Comments