Mkuu
wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amewataka wazazi na walezi mkoani Rukwa kuwalea
watoto wao katika malezi bora na kujiepusha na vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo
sambamba na kujiepusha na migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikijitokeza na kusababisha
tatizo la watoto wa mitaani.
katika picha ni baadhi ya watoto wakipatiwa elimu na shirika la bethaniaa juu ya umuhimu wa haki zao |
Chimbuko la haki za mtoto lilitokana na mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto ulioidhinishwa na Nchi wanachama wa umoja wa mataifa mnamo novemba 20,1989 na kuridhiwa na serikali ya jamhuri ya mungano wa Tanzania Juni10,1991.
Hata
hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa
haki za watoto umoja Afrika
ulipitisha mkataba wa afrika wa haki na
usitawi wa mtoto mwaka 1990 na huku mkataba huo ukilenga kuhakikisha kuwa
mkataba wa kimataaifa wa haki za mtoto unatekelezwa kwa kuzingatia mila ,desturi,na tamaduni za
kiafrika .
katika picha ni mkuu wa wilaya ya kalambo |
Akizindua mradi wa kutambua haki za watoto uliokuwa umeandaliwa na shirikia la Future and Hope-(BETHANIA HOMES), mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura amesema wazazi na walezi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao wanaendelezwa katika nyanya za kielimu,kimaadili,na kiimani.
‘‘niwasihi
wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapewa nafasi ya kushiriki na
kushirikishwa katika masuala yanayowahusu ikiwa ni pamoja kutoa maoni
,kusikilizwa na kushiriki katika maamuzi
mbalimbali katika familia na jamii kwa ujumla ‘’alisema Binyura.
Amesema
katika
sheria ya mwaka 2009 mtoto
anahaki mbalimbali katika
jamii ikiwemo kupata haki ya
kuishi,kupumzika kuheshimiwa na kuthaminiwa.
katika picha ni mratibu wa Shirika la Bethania akitoa elimu kwa wananchi |
Joseph
Kasaila mratibu wa tasisi ya Future and Hope –BETHANIA HOMES,amesema wamelazimika
kupeleka mradi huo utahudumu katika eneo la Matai wilayani kalambo na
kusema lengo kubwa ni kuhakikisha
wananchi wanapata ulewa juu ya umuhimu wa kuwalea watoto kwa lengo la kupunguza
wimbi la watoto wa mitaani.
‘’mfano
watoto wanao pitia adha hiyo
ni wanaopitia hali hii ni wale ambao waliofiwa na wazazi wote
wawili(yatima) watoto wanaohusishwa na huduma za kingono kinyume na
sheria ,watoto wanaofanya kazi mogodini ,watoto wanaokinzana na sheria
,watoto wanaoishi na kufanya kazi
mitaani ,watoto wenye ulemavu na watoto
wenye mambukizi ya VVU na UKIMWI.’’alisema
Kasaila
katika picha ni kaimu mkurugezi akitoa elimu kwa wananchi |
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo yasita Nkyabonaki,amesema kila mzazi anatakiwa kuhakikisha waatoto wanalelewa katika misingi bora na tabia njema.
‘’marekebisho yanaanziakatika ngazi ya familia
na jamii ,ambapo wazazi /walezi na wanajamii wanajukumu kubwa la kuhakikisha
kuwa kila mtoto analelea na kukua kwa
kufuata maadili,mila ma destruri za jamii husika.’’alisema Nkyabonaki.
Comments
Post a Comment