Katika picha ni katibu tawala wilayani kalambo |
Uongozi wa serikali wilayani Kalambo mkoa wa Rukwa umewaagiza
watumishi wote wa umma wilayani humo kusajili laini za simu zao za
mitandao mbalimbali kwa njia ya alama za vidole ili kuimarisha utendaji
wao bora wa kazi.
Akizindua zoezi la mkakati wa kusajili laini za simu
wilayani kalambo katibu
tawala wilayani wilayani humo Frank Sichalwe, amesema usajili
huo utawawezesha watumishi hao kutoa huduma inayostahili kwa wakati unaostahili
na kusaidia kuchochea shughuli za maendeleo ya jamii.
Amesema zoezi hilo litatawahusu watu wote kutoka maeneo ya
vijijini na mijini na kusema kwa
sasa wameanza na watumishi wote
wilayani humo kwa kupatia elimu.
Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa matai wilayani kalambo mkoa
wa Rukwa wameelezea
umuhimu wa kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole na kusema
utaratibu huo utalinda usalama wa mteja kutokea uwezekano wa kufanyiwa
vitendo vya uhalifu na watu wenye nia ovu.
Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano-tcra- kanda ya nyanda za juu kusini mhandisi Asajile John, amesema lengo
la serikali katika kutekeleza zoezi hili ni kutoa wigo mpana wa kuthibiti
uhalifu wa mtandaoni na kuthibiti matumizi mabaya ya simu ambapo kawia ntemo afisa usajili kutoka
mamlaka ya vitambulisho vya taifa-nida-anaelezea
changamoto zilizopo.
mamlaka ya mawasiliano-tcra- kanda
ya nyanda za juu kusini inaendesha zoezi la kuhamasisha usajili wa laini za
simu kwa njia ya alama za vidole katika mikoa ya Rukwa na Katavi kabla
ya ukomo wa zoezi hili mwezi december mwaka
huu
Comments
Post a Comment