Na Israel Mwaisaka,Nkasi
![]() |
Baadhi ya mashabiki wa simba wakitoa misaada watoto yatima. |
Wanachama wa club ya simba wilayani Nkasi mkoani Rukwa wametoa
msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha kilangala mission kama njia ya
kusherehekea wiki la simba day.
Akikabidhi msaada huo kwaniaba ya wanachama hao wa simba donal
mkama alisema kuwa msaada huo walioutoa wa vitu mbalimbali una thamani ya zaidi
ya tshs,500,000 na fedha hizo zimetokana na michango mbalimbali kutoka kwa
wanachama.
alisema kuwa wao kama tawi la simba wilayani Nkasi walikaa na
kutafakari nini cha kufanya katika wiki hili la simba day na wakaonelea kuwa
kuna umuhimu wao kwenda kuungana na watoto yatima katika kituo cha kilangala
ambao wanapata tabu sana kutokana na mazingira nagumu waliyonayo.
alifafanua kuwa wanachama wote kwa ujumla walikubaliana kuwa wao
kama marafiki wa simba wanalojukumu la kufanya siku hiyo kwa jamii na kila
mmoja aliguswa na ambavyo watoto yatima wanavyokabiliwa na changamoto
mbalimbali na kuamua kuchanga fedha ili kutoa msaada kwa kituo hicho.
Albert Nayingo mmoja wa wanachama hao amedai kuwa wao kama
wanachama wa simba wataendelea kufanya shughuli mbalimbali za
kijamii hata kama wiki la simba day litakwisha kwani club yao imelenga
kuwasaidia jamii kutokana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
kwa upande wake Francis Mkemwa alidai kuwa kwa sasa club yao ina
wanachama wengi na hivyo wanao mfuko mkubwa na kuwa fedha walizozitoa ni sehemu
tu ya zile zilizopo kwenye mfuko wao na kuwa lengo lao sasa ni kuendelea
kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuweza kuisaidia jamii
yenye shida.
Akipokea msaada huo msimamizi msaidizi wa kituo cha watoto yatima
kilangala Mission Velonica wakalanda aliishukuru club ya simba tawi la nkasi
kwa uamuzi huo wa kuwapelekea msaada huo na kuwa kwa kipindi hiki walikua na
Comments
Post a Comment