Na baraka lusajo. Kalambo.
katika picha ni mwenyekitri wa ccm wilaya ya kalambo. |
Chama
cha mapindizi CCM wilayani Kalambo mkoani Rukwa kimeipongeza ofisi ya mkuu wa
wilaya hiyo kwa kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya umaliziaji wa
maboma pamoja na ukarabati wa majengo ya shule na zahanati .
Ofisi
ya mkuu wa wilaya ya kalambo imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kila mwaka
kulingana na uhitaji wa maeneo husika,ambapo kwa mwaka huu iilitoa vifaa vya ujezi
ikiwemo bati na saruji na kuwakabithi watendaji
na madiwani kwa lengo la kusaidia umaliziaji wa majengo kwenye kata na vijiji tofauti vilivyopo wilayani humo.
Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi CCM wilayani humo Alfred Mwanga amesema kwa ujumla ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo nimekuwa
ikijitahidi kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za wananchi hususani maeneo ya vijijini.
‘’tunakupongeza
kutoa misaada hii,lakini madiwani wapo, watendaji wapo,wenyeviti wa vijiji
wapo hivyo sitegemei kuona eti sikumoja
unapewa taarifa kuwa misaada ulitoa
haikutumika vile inavyotakiwa na wakati wahusika wote wapo itakuwa ni majabu
‘’alisema Mwanga.
Mbali
na hayo amelaani vikali kitendo cha baadhi ya viongozi kuto unga mkono jitihada
zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya mungano waTanzania John Paombe Maghufuli nakusema watu hao si wema katika taifa hili.
katika picha ni mkuu wa wilaya ya kalambo akitoa misaada |
Mkuu
wa wilaya hiyo Julieth Binyura amewataka wananchi pamoja na wachungaji
kuendelea kumuombea Rais Wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayo ifanya
.
Hata
hivyo kwa mwaka 2019 ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo imetoa misada ya vifaa vya ujezi kwa mashirika ya dini,watu
binafus pamoja na kwenye taasisi ya za serikali vyote vikiwa na thamani ya
shilingi milioni tano.
Comments
Post a Comment