Bobi Wine : Ashtakiwa kwa kumkasirisha na kumkejeli rais Yoweri Museveni

Bibi Wine hivi karibuni alitanagaza kwamba atawania urais 2021Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mbunge wa Uganda na mwanamuziki Bobi Wine ameshtakiwa kwa lengo la kumkasirisha, na kumkejeli rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Mbunge huyo na wenzake wametuhumiwa kwa kuurushia mawe msafara wa rais wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa kaskazini wa Arua 2018.
Shtaka hilo jipya limeongezwa katika shtaka jingine la uhaini dhidi ya mbunge huyo.
Iwapo atapatikana na hatia Wine atakabiliwa na kifungo cha maisha jela.
Wine na wenzake wengi wanasema kwamba waliteswa wakati walipokuwa kizuizini, kitu ambacho mamlaka imekana.
Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulani bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyengine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za rununu 2018.
Msanii huyo ambaye amekuwa mwanasiasa wa upinzani anayepinga utawala wa miongo mitatau ya rais Museveni hivi majuzi alitangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi wa 2021.
Tayari amezindua kikosi kitakachoendesha kampeni yake ya kuwania urais 2021.
Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kama changamto kwa Yoweri Museveni.
Museveni, mwenye umri wa miaka 74, anatarajiwa kuwania muhula wa sita madarakani.
Msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya uhaini baada ya kukamatwa mwaka jana kufuatia kupurwa mawe msafara wa rais baada ya mkutano wa kisiasa.
Aliliambia gazeti la Financial Times kwamba zaidi ya wabunge 50 , ikiwemo 13 kutoka kwa chama tawala cha rais Museveni cha National Resistant Movement NRM waliunga mkono ugombeaji wake na hivyobasi kumpatia ujasiri wa kuogombea kiti hicho.

Ufuasi wa Vijana

Wine anasema Museveni hazingatii maadili yaliomuongoza kwa wakati mmojaHaki miliki ya pichaAFP
Mchambuzi wa kisiasa Nicholas Sengoba anasema uchaguzi mdogo wa Arua ulioshindwa na mgombea aliyeungwa mkono na Wine ulikuwa ni wa 'kufa au kupona kwa Museveni'.
"Chama chake kitawaza iwapo sasa huu ni msururu. Bobi Wine sasa amemshinda Museveni na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye mara nne'' katika uchaguzi mdogo.
"Bobi amepata ufuasi kwa nembo yake ya 'nguvu za watu', na ananuia kushinikiza na kupanga liwe vuguvugu," anaongeza.
Mchambuzi wa kisiasa Robert Kirunda anasema mvuto wa Wines unatokana na kuwepo 'pengo la uongozi' Uganda.
"Kuna vijana wengi Uganda ambao hawana haja ya kujua vita vya kihistoria vilivyoiingiza NRM uongozini, au ukaidi wa upinzani mkuu. Wengi wanataka ajira na wanahisi uchumi hauwasaidi."
Kirunda anasema Wine 'anapigia upatu sana'. "Anaweza kushinikiza watu pakubwa, lakini bado hajapata nguvu kama alizonazo Besigye katika upinzani".

Comments