Bingwa wa mita 800 duniani David Rudisha ahusika katika ajali mbaya ya barabarani Kenya

David Rudisha ahusika katika ajali mbaya ya barabarani
Bingwa wa mbio za mita 800 anayeshikilia rekodi ya dunia David Rudisha anaendelea kupata matibabu kufuatia ajali mbaya ya barabarani ilimuacha akiuguza majeraha .
Bwana Rudisha alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota V8 siku ya Jumapili alfajiri ambapo tairi lake lilipasuka karibu na mji wa Keroke na hivyobasi kugongana ana kwa ana na basi moja lililokuwa likitokea upande wa pili.
Ajali hiyo ya mwendo wa saa nne na nusu ilitokea katika eneo hatari katika barabara kuu ya Kisii Keroka kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.
Bwana Stephen Ole Marai ambaye ni rafiki a Rudisha na jirani alisema kwamba hali ya mwanariadha huyo haipo hataraini na alitibiwa katika hospitali moja iliopo Keroka kabla ya kuhamishwa katika hospitali ya Kilgoris.
Katika mitandao ya kijamii Wakenya walimwambia pole Rudisha huku wakiweka picha za gari lake lililoharibika vibaya

Comments