Katika picha ni mkuu wa wilaya ya Nkas Said Mtanda |
Mkuu wa Wilaya ya
Nkasi Mh. Said Mtanda amewatahadharisha kinababa wenye tabia ya kunyonya maziwa
ya kinamama wanaonyonyesha kwani hicho ni chakula maalum kwaajili ya mtoto
aliyezaliwa na yeyote anayefanya hivyo anadhulumu haki ya mtoto ambaye
hutegemea maziwa ya mama kwa muda wa miezi sita bila ya kula chakula cha aina
yoyote.
Amesema kuwa kazi
kubwa ya kinababa ni kuwawezesha kinamama kupata lishe bora ili waweze kuwa na
afya thabiti kutoa maziwa ya kutosha na kuweza kuwa nyonyesha watoto wao na
kuongeza kuwa katika mkoa wa Rukwa asilimia 81 ya watoto wenye umri
chini ya miezi sita wanalishwa vyakula vingine vya ziada, jambo ambalo
halikubaliki kwa maendeleo ya mtoto.
“Ujumbe
wa Leo ni kwamba watoto wadogo chini ya Miezi Sita ndio wanaotakiwa
kunyonyeshwa, kwahiyo kinababa na wao wenye kupenda maziwa ya baba waache
kwasababu hicho sio chakula chao ni lishe kwa watoto wachanga, tusidhulumu haki
za watoto za unyonyeshaji, tuache tabia ya kunyonya maziwa ya mama kwa wasiohusika,”
Alisisitiza.
Aidha
alisema kuwa tafiti zinaonesha kuwa asilimia 17 ya watoto wenye umri chini ya
miezi 6 wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa kinywaji au chakula
kingine kama inavyoshauriwa na Shirika la Afya Duniani. Hii ina maana kuwa asilimia
83 ya watoto wenye umri huo hawanyonyeshwi ipasavyo.
Mh. Mtanda aliyasema
hayo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kimkoa katika
Kijiji cha Kisumba, kilichopo Wilaya ya Kalambo akimwakilisha aliyetakiwa kuwa
mgeni rasmi wa uzinduzi huo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
katika picha ni kaimu katibu tawala mkoani Rukwa Albinus Mgonya |
Kwa upande wake Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya aliisifu timu ya afya ya Mkoa kwa
kuwezesha kufanyika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji katika
Kijiji cha kisumba kutokana na Kijiji hicho kuwa na kinamama wengi
wanaonyonyesha.
“Katika Kijiji hiki
Mheshimiwa mgeni rasmi kuna Kaya 1300, na kwa takwimu ambazo tunazo kupitia
idara yetu ya afya kinamama wanaonyonyesha watoto katika Kijiji hiki cha
Kisumba ni 234, hivyo utaona kwamba tumekuja kuhakikisha kuwa ujumbe huu
unafika kwa wadau kwa njia muafaka,” Alieleza.
Halikadhalika alisema
kuwa maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na utekelezaji wa mradi wa Lishe
Endelevu unaolenga kuongeza idadi ya watoto wenye umri kati ya miezi 6 – 23
kuhakikisha kwamba wanapata vyakula vyenye mchanganyiko sahihi na kusisitiza
kuwa ni muhimu kinababa kushiriki katika maadhimisho hayo ili wawe msaada
mkubwa kwa kinamama.
Katika picha ni katibu tawala wilaya Kalaambo Frank Sichalw akiongea na wananchi wa kijiji cha kisumba |
Katibu tawaala wilayani
humo Frank Sichalwe aliwasisitiza
akinamama kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama huchangia kwa kiasi kikubwa katika
kuboresha afya, kulinda uhai na maisha ya mtoto.
Asilimia 67 ya watoto wa umri kuanzia miezi 6
– 23 wanapewa vyakula ambavyo havina mchanganyiko wa kutosha, yaani mlo
usiokamilika, hali inayodhihirisha kuwa, taratibu duni za ulishaji watoto ni
mojawapo ya sababu za utapiamlo katika Mkoa wa Rukwa.
Baadhi ya wananchi katika maadhimisho ya unyonyeshaji |
Kalambo mambo ni faya
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete