katika picha ni waziri wa mambo ya ndani kangi lugora. |
Na Baraka lusajo .Rukwa.
WAZIRI wa Mambo ya ndani
ya Nchi Kangi Lugola ameahirisha ziara yake mkoani Rukwa iliyokua imeanza leo
kutokana na ajali iliyotoke leo alfajiri mkoani Morogoro .
Akizungumza na Waandishi
wa habari mjini Sumbawanga amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa
kamishina jenerali wa jeshi la zima moto Thobias Andengenye juu ya
ajali iliyotokea mjini Morogoro katika maeneo ya Msamvu ikihusisha
gari la mafuta na kuua watu kadhaa .
Alisema kuwa ajari hiyo
iliyotokea imehusisha Watu wengi na ambao idadi yake bado hajaipata sawasawa na
kuwa kutokana na mazingira hayo ameamua kuiahirisha ziara hiyo
mkoani Rukwa ili aweze kwenda kuungana na watanzania wengine juu ya msiba huo
mkubwa.
Alidai kuwa bado kuna
tatizo kubwa la matumizi ya barabara kwa watu wote na kuwa kama sheria ya
Usalama barabarani Sura 168 itatumika sawasawa kwa watumiaji wa
barabara kuna uwezekano mkubwa wa ajali kama hizo zikaweza kuepukwa.
Lugola alifafanua kuwa
licha ya sheria hiyo ya usalama barabarani kuwepo serikali ipo kwenye mchakato
wa kuitunga sheria mpya ya Usalama barabarani na kuwa sheria hiyo mpya ipo
mbioni na itaanza kufanya kazi ili kuweza kukabiliana na ajali zisizokuwa za
lazima na kuweza kupoteza maisha ya watu wasiokua na hatia.
Alidai kuwa jeshi la
Polisi mkoani Morogoro limefanya kazi kubwa ya kuwatawanya watu
waliokuwa katika eneo la tukio vinginevyo hari ingekua mbaya zaidi na kutoa
wito kwa jamii kutokimbilia katika maeneo yanapotokea majanga hususani ya moto
kama ilivyokuwa mkoani morogoro .
katika picha ni mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo. |
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Rukwa
Joachim Wangabo ametuma salamu
za rambirambi kwa mkuu wa mkoa
wa morogoro kufuatia
kujitoza kwa ajali
hiyo.
Comments
Post a Comment