WATU WATATU WAKAMATWA NA RISASI 1493 ZA KIVITA WILAYANI NKASI

Na Baraka Lusajo - Rukwa 

Jeshi la polisi mkoani Rukwa limeripoti matukio mawili tofauti likiwemo la watu 5 kukamatwa na risasi 1493 za silaha za kivita aina ya AK 47 na SR huku watu wawili kati ya hao wakikamatwa na risasi 14 za Shotgun pamoja na vipande 31 vya gamba la kobe kinyume na sheria.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa ACP William Mwampagale alisema baada ya kupata taarifa fiche kwa kushirikiana na raia wema walifanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na risasi 1493 za silaha za kivita aina ya Ak 47 na SAR kinyume cha sheria.


Alisema katika uchunguzi wa awali walibaini kuwa wavuvi 7 walizikuta risasi hizo zikiwa mapangoni wakidhani ni madini ya dhahabu.

‘’Watuhumiwa hao walikamatwa na walipohojiwa walishindwa kuelezea walikuwa wanazipeleka wapi ingawaje walizitambua kuwa ni risasi za moto. upelelezi wa kina Zaidi unaendelea ili kubaini nia yao’’ alisema kamanda Mwampagale

Aidha katika tukio la pili jeshi hilo linawashikilia watu wawili baada ya kuwakamata katika eneo la Kashai Edeni ‘’B’’ kata ya Momoka manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa na kwamba walipatikana wakiwa na risasi 14 za shotgun.


‘’Pia watu hao walipatikana wakiwa na vipande 31 vya gamba la kobe pamoja na nyamapori vipande viwili, manyoya nungunungu vipande  2  na mishale 2 ambayo huwawezesha katika kutekeleza vitendo vya ujangili.Watuhumiwa hawa watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

 

Comments