Na Baraka Lusajo-Rukwa.
Mamlaka ya Bandari
hapa nchini imeanza utekelezaji
wa miradi mitatu ya bandari katika Mkoa wa Rukwa inayogharimu kiasi cha
shilingi bilioni 12 .7 katika ya kalambo
na Nkasi.
katika picha ni eneo laa ujezi wa bandari wilayani Nkas. |
Akingea wakati
wa ukaguzi wa mradi
huo, mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo amesema kuna kila
sababu ya wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha
ukarabati wa meli ya MV Liemba ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na
wananchi wanaoishi
Mh. Wangabo amesema
kuwa wananchi hao wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutumia vyombo kama
mitumbwi na boti ambavyo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na meli kubwa ya
MV Liemba ambayo usalama wake ni wa uhakika.
“Nitoe wito kwa wizara
husika hii meli ya MV Liemba nimeambiwa hapa kwamba ikipita kwenda Zambia
inaitwa ‘Our Baby’ mtoto wetu, sasa huyu mtoto wetu anaulizwa yuko wapi, Zambia
wanauliza, sasa Wizara husika twende haraka isimamie hili jambo, MV Liemba
itengenezwe, watu maisha yao yapo kwenye hatari kubwa ndani ya hili ziwa
Tanganyika”
Naye Mbunge wa jimbo
la Nkasi Kaskazini Mh Ali Kessy alieleza kuwa meli hiyo ya MV Liemba ilitakiwa
kukamilishwa ukarabati wake tangu mwaka wa fedha 2017/2018 lakini fedha za
ukarabati hazikutengwa na kudai kuwa Waziri wa Fedha Mh. Filipo Mpango
amemuhakikishia kuwa fedha za ukarabati wa meli hiyo zimetengwa katika bajeti
yam waka 2018/2019.
Kwa upande wake Meneja
wa Bandari za Ziwa Tanganyika Pasivo Ntetema amesema kuwa mradi huo unahusisha
ujenzi wa gati, jengo la kupumzikia abiria, jengo la mgahawa, ofisi, ghala la
kuhifadhia mizigo, nyumba za wafanyakazi na uzio na kuongeza kuwa kwa Bandari
ya Kabwe peke yake wastani wa usafirishaji kwa mwezi ni tani 1500 hadi 2000 na
mwaka wa fedha 2018/2019 zimesafirishwa tani 20,000
“Pamoja na changamoto
za miundombinu lakini utaona kuna ‘access’ nzuri ya watu kupita hapa kwahiyo
kukishaboreshwa bandari hii ikakamilika lakini pia miundombinu ya barabara ya
kuingia hapa ikakamilika ni Imani yetu watu wa bandari ya kwamba kupitia
uongozi wako, kupitia mheshimiwa mbunge na mamlaka zote zinazotawala mkoa wa
Rukwa pamoja na serikali kuu, tutaangalia sasa uwezekano wa kuboresha barabara
hii kwa kiwango cha lami ili shehena kubwa iweze kupita hapa
Mamlaka ya Bandari
inatekeleza miradi mitatu katika Mkoa wa Rukwa ambayo ni Mradi wa uboreshwaji
wa bandari ya Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo, Ujenzi wa barabara katika
Bandari ya Kipili na Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Gati Bandari ya Kabwe
zilizopo katika Wilaya ya Nkasi ambapo miradi yote itagharimu shilingi bilioni
12.7
Comments
Post a Comment